• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

WAGANGA WAKUU WAMKABIDHI RAIS TUZO MAALUM — MHE. MPANGO ATOA MAELEKEZO YA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA.

Posted on: July 12th, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake kwenye Sekta ya Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri hii leo.

Tuzo hiyo ameitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Waganga hao na kumkabidhi Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philipo Mpango aliyekuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri jijini Dodoma.

Pia, Waganga Wakuu wamemtunukia Makamo wa Rais tuzo hiyo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe Mohamed Mchengerwa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama.

Mhe. Mpango amewapongeza Waganga Wakuu nchini kwa kazi wanayofanya ya kuwahudumia wananchi huku akiwataka waendelee

kuimarisha huduma na sekta ya afya kwa ujumla na kuzingatia maadili ya taaluma yao.

Amesisitiza kuwa Serikali itatekeleza mara moja maombi ya kuboresha stahili za wataalam hao kulingana na hali halisi ya uchumi.

"Nawaelekeza Mawaziri wa Afya na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha washughulikie suala la ucheleweshaji wa posho za madaktari na wahudumu wa afya." Amesisitiza Mhe. Mpango

Amesema kwa sasa Serikali inapoelekea kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kuhakikisha zinasimamia vema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika kiadilifu ili kuboresha zaidi utoaji wa huduma.

Pia amewapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri/Manispaa na Majiji kwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ile ya afya na vifaa tiba katika Halmashauri/Manispaa/Majiji.

Amesema ili kuimarisha huduma za afya na usimamizi shirikishi, Serikali imenunua na kusambaza magari ya kubeba wagonjwa (ambulance) na mashine za kisasa za kidijiti (Digital X-ray na ultrasound) na kuagiza kuvitunza vifaa hivyo na vingine vitakavyonunuliwa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa watu wengi zaidi.

Naye, Mhe.Mchengerwa amemshukuru Rais Samia kwa maono na miongozo yake kwenye sekta ya Afya yaliyopelekea mageuzi makubwa.

Matangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI. April 25, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DC KILWA AZINDUA STENDI KUU YA MABASI NANGURUKURU.

    July 21, 2025
  • KAMATI YA HUDUMA ZA MIKOPO KILWA YAFANYA KIKAO MAALUM KUHAKIKI VIKUNDI VYA WAOMBAJI MIKOPO.

    July 15, 2025
  • WAGANGA WAKUU WAMKABIDHI RAIS TUZO MAALUM — MHE. MPANGO ATOA MAELEKEZO YA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA.

    July 12, 2025
  • KILWA YAPOKEA PIKIPIKI 11 KWA AJILI YA CHANJO NA HUDUMA MBALIMBALI ZA MIFUGO.

    July 11, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa