Kilwa,
Wafanyakazi wa sekta za umma na binafsi wametakiwa kujiandaa kiuchumi kabla ya muda wao wa kustaafu haujafika.
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi alipokua akihutubia mamia ya wananchi na wafanyakazi kutoka katika taasisi mbalimbali katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani kwa Mkoa wa Lindi yaliyofanyika katika viwanja vya Garden Mkapa Mjini Kilwa Masoko.
Zambi maesema ni vyema wafanyakazi wakajiandaa kwa kutengeneza mazingira mazuri ambayo wataishi pindi watakapokua wamestaafu
“Ndugu yangu ukitegemea mafao yako utakayopata ndio uyatumie kwa kujengea nyumba ya kuishi na kuanzishia shughuli zingine za kukuingizia kipato utakuja kufa mapema baada ya kustaafu, ni vyema ukaanza kubana bana fedha zako sasa na kuanzisha miradi ya kimaendeleo ambayo itakusaidia hata baada ya utumishi wako kufika kikomo” alisema Zambi.
Pia Mhe. Zambi amewataka waajiri kuwaruhusu wafanyakazi kuafanya Mabaraza yao ambayo yatasaidia kumaliza baadhi ya migogoro ambayo inawakabili na kujadiliana mambo mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku
“Waajiri muwaache wafanyakazi wakutane kwa mujibu wa sheria wajadiliane mambo yao. Lakini na ninyi wafanyakazi sio mnakutana tu ili mradi mnakutana hata kama hamna ajenda ya maana katika mikutano hiyo na mkageuza kua vijiwe vya kujadili umbea na mambo yasiyokuwepo”alisistiza Zambi.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani kwa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akimkabidhi zawadi ya mmoja wa wafanyakazi bora katika maadhidhimisho yaliyafanyika katika viwanja vya Garden Mkapa mjini Kilwa Masoko ( Picha na Ally Ruambo)
Adha Zambi amewataka waajiri kuandaa Taarifa za watumishi ambao wanakaribia kustaafu mapema ili muda wa kustaafu unapofika wapate stahiki zao haraka kutoka katika mifuko ya Hifadhi ya jamii ambayo mtumishi amejiunga
“Tunaweza kua tunalalamikia mifuko kuchelewesha kulipa mafao kwa watumishi wanaostaafu kumbe waajiri nao wanaweza kua ni chanzo kwa kuchelewesha kuandaa na kuwasilisha taarifa za watumishi wanao staafu” alisisitiza Zambi.
Awali akitoa salamu za wilaya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai ameshukuru kwa Wilaya ya Kilwa kupewa Hadhi ya kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani kwa Mkoa wa Lindi na kuwataka Wafanyakazi wafanye kazi kwa weredi na kuzingatia maadili ya kiutumishi.
Sanjari na burudani kutoka katika vikundi mbalimbali, wafanyakazi kadhaa kutoka katika taasisi mbalimbali mkoani Lindi na Halmashauri zake walipewa zawadi za ufanyakazi bora
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa