Wadau wa mazingira Wilayani Kilwa mkoani Lindi wakiwemo Tanzania Agroforestry and Marine Conservation Organization (TAMCO), Afri Craft na Kikundi cha Umoja wa Wapanda Mikoko (UWAMIKO), kwa kushirikiana na wataalamu wa Mazingira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la usafi wa fukwe za bahari. Zoezi hili limefanyika kwa lengo la kuhakikisha fukwe zinakuwa safi na zenye kuvutia.
Zoezi hili limefanyika tarehe 27 Agosti 2025, katika fukwe ya jimbiza kata ya Masoko ambapo wadau hao washiriki wamekusanya taka mbalimbali na plastiki zilizokuwa zimetapakaa katika fukwe hizo na kuhakikisha maeneo hayo yanabaki safi na salama.
Kupitia ushirikiano huo wadau wamejifunza athari za kutotunza mazingira ya bahari ikiwemo kupungua kwa rasilimali za bahari kutokana na plastiki ambazo zinapelekea udumavu wa mazalia ya bahari ikiwemo samaki jambo linalopelekea kushuka kwa uchumi wa jamii zinazotegemea kipato kutokana na shughuli za uvuvi.
Pia wamejifunza namna ya utunzaji wa mazingira ya fukwe unvyoweza kuvutia kufanya shughuli za utalii wa fukwe kwa jamii kutoka sehemu mbalimbali jambo ambalo litasaidia jamii ya Kilwa kujipatia kipato kupitia shughuli hizo.
Ushirikiano huu pia unaonyesha jinsi sekta za kijamii, mashirika ya mazingira, na serikali zinavyoweza kushirikiana kwa ufanisi ili kudumisha rasilimali za bahari kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo upandaji mikoko na usafi wa mazingira ya bahari.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa