Kuelekea zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura, Waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki katika jimbo la Kilwa Kusini na Kilwa Kaskazini wamepewa mafunzo ya muda wa siku mbili ili yawajengee uwezo katika katekeleza majukumu yao. Kwa upande wa jimbo la Kilwa Kusini Mafunzo yamefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilwa na Jimbo la Kilwa Kaskazini mafunzo yamefanyika Katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ilulu Tarehe 25 -26 Januari 2025.
Akifungua mafunzo hayo Afisa Mwandikishaji Jimbo la Kilwa Kusini na Kilwa Kaskazini Ndg. Msena Bina, amewasisitiza waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki kuwa, vifaa watakavyokabidhiwa vitunzwe ili kufanikisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.
Aidha, Ndg. Bina ameeleza kuwa lengo la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni kuandikisha wapiga kura wapya ambao tayari wana miaka 18, au wale watakokuwa na miaka 18 kabla au ifikapo siku ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuhamisha taarifa za watu waliohama makazi, kurekebisha taarifa zilizokosewa, kutoa kadi mpya kwa watu waliopoteza kadi au kuharibika, Lakini pia kuondoa taarifa za watu waliopoteza sifa za kupiga kura.
Uboreshaji wa daftali la kudumu la wapiga kura katika jimbo la Kilwa Kusini na Kilwa Kaskazini litaanza rasmi Januari 28, 2025 hadi Februari 3, 2025 ambapo kauli mbiu ya zoezi hili ni :
"Kujiandikisha kuwa Mpiga kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa