Kilwa,
Mkuu wa polisi wilaya ya kilwa H. Banzi amevitaka Vyama vya ushirika wilayani kilwa kutoa taarifa mapema pindi wanapopata Matatizo.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi za Vyama vya Ushirika pamoja na Makatibu wa Vyama hivyo katika ufunguzi wa Mafunzo yanayoendelea katika Ukumbi wa kwa Sultan Mjini Kilwa .
Banzi amesema Vyama vya Ushirika vimekuwa vikichelewa kutoa taarifa pindi yanapotokea matatizo katika Vyama vyao hasa inapotokea mkanganyiko katika masuala ya Kifedha.
Amesema kuna kesi nyingi ambazo zimekuwa zikiziripotiwa Polisi baada ya muda mrefu kupita, muhusika kukimbia au zikiwashinda kuzimaliza.
“Utakuta tukio limetokea miezi kadhaa nyuma lakini mnakaa kimya mpaka muhusika anatoroka au mnashindwa kulipatia ufumbuzi ndio mnkuja kutoa taarifa , halafu watu wakihoji mnasema tusharipoti Polisi wanalifanyia kazi” alisema Banzi
Pia amevitaka vyama vya ushirika kuchagua watunza fedha wenye ujuzi ili kupunguza matatizo ambayo yanaweza kuepukika.
Banzi amesema polisi imekuwa ikipokea kesi nyingi kutoka Vyama vya ushrika kuwa kuna baadhi ya Viongozi wamekula pesa kitu ambacho muda mwingine kinakuwa hakina ukweli
“Kuna kesi ilikuja kwamba kuna Mtu amekula Pesa ya Chama ambayo ilikuwa karibia milioni Mia Moja lakini kwa kushirikiana na Takukuru tukafuatilia na kugundua kuwa hakuna pesa iliyokuwa imeliwa ni makosa tu yalikuwa yamefanywa na walikuwa wanaendesha zoezi kutokana na kukosa ujuzi wa usimamizi wa fedha, katika milioni Mia Moja karibia milioni Themanini zilipatikana” alisema Banzi
Wajumbe wa Bodi za Vyama vya Ushirika pamoja na Makatibu wakiwa katika Mafunzo yanayoendelea katika Ukumbi wa kwa Sultan Mjini Kilwa
Naye mtunza Ghala, Ghala la Nangurukuru Ndg. Mbaraka Makolongo amesema maandalizi kwa ajili ya Msimu wa Korosho yanaendelea vizuri na kusema kuwa kuanzia Oktoba 17 watakuwa tayari kuanza kupokea Korosho.
Pia amewatoa hofu Wakulima kuhusu Nafasi ya kuhifadhia mazao yao baada ya kufika ghalani kwani nafasi ipo ya kutosha.
“Chamgamoto ya Nafasi tulisha ifanyia kazi kwa msimu huu hakutakuwa na changamoto hiyo tena kwahiyo niwaombe tu wakulima walete Korosho zao, Lakini wahakikishe korosho wanazoleta zina ubora unotakiwa” alisema Mbaraka
Awali akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujifunza kwa bidii na kwenda kuyafanyia kazi yale watakayo fundishwa.
“Baada ya mafunzo haya hatutarajiiu kuona makosa ambayo yalikuwa yakifanyika siku za nyuma yanajirudia tena, sasa hivi mutakuwa na ujuzi ambao utasaidia katika kuboresha kazi zenu kwahiyo hatutarajii kusikia makosa yamejirudia.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa