Kuelekea zoezi la uboreshaji wa daftrai la kudumu la wapiga kura katika Wilaya ya Kilwa litakalofanyika kwa muda wa siku saba (7) kuanzia tarehe 28/01/2025 hadi 03/02/2025. Afisa mwandikishaji katika Wilaya ya Kilwa Ngd. Msena Bina , amengoza kikao na Viongozi wa Vyama vya Siasa ili kuwataarifu juu ya umuhimu wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, kikao kimefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Kilwa, Tarehe 22/01/2025.
Ndg. Bina ameeleza kuwa lengo la uboreshaji wa daftrai la kudumu la wapiga kura ni kuandikisha wapiga kura wapya ambao tayari wana miaka 18, au wale watakokuwa na miaka 18 kabla au ifikapo siku ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, kuhamisha taarifa za watu waliohama makazi, kurekebisha taarifa zilizokosewa, kutoa kadi mpya kwa watu waliopoteza kadi au kuharibika, Lakini pia kuondoa taarifa za watu waliopoteza sifa za kupiga kura.
Aidha, amewasisitiza Viongozi wa Vyama vya Siasa kutoa hamasa kwa wananchi walioko katika maeneo yao ili waweze kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao. Vituo vya uandikishaji vitafunguliwa kuanzaia saa 02: 00 Asubuhi hadi saa 12:00 Jioni kwa kila kituo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa