Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, Viongozi wa dini Wilayani Kilwa wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha jamii juu ya ulinzi, ustawi na maendeleo ya watoto ili kuwawezesha kufikia malengo yao na kujenga taifa lenye misingi bora ya haki na usawa.
Wito huo umetolewa na Afisa Tarafa ya Pwani, Ndg. Mfaume Sudi, akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Maadhimisho hayo yamefanyika tarehe 16 Juni 2025 katika uwanja wa Mkapa, Kilwa Masoko. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa “Haki za Mtoto: Tulipotoka, Tulipo na Tuendako.
Pia Ndg. Sudi ameisisitiza umuhimu wa jamii, hususani wazazi na viongozi wa dini, katika kuhakikisha watoto wanatunzwa, kulindwa dhidi ya ukatili, na kupewa fursa sawa za kupata haki zao za msingi kama elimu, afya na malezi bora.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa maendeleo ya jamii wakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali kama ActionAid, TCRS, TUJIWAKI, pamoja na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Wadau hao walitoa ujumbe wa hamasa na kuhimiza jamii kutoruhusu ukiukwaji wa haki za watoto kufumbiwa macho, bali wawasilishe malalamiko kwa mamlaka husika kwa ajili ya hatua stahiki.
Aidha, tukio hilo limepambwa na burudani mbalimbali zilizotolewa na watoto, zikiwemo ngoma za asili, mashairi, maigizo na nyimbo zilizobeba ujumbe wa kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutetea na kulinda haki za watoto.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa