Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro amewahasa wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Kilwa, kuendelea na nidhamu waliyokuwa nayo shuleni hata baada ya kuhitimu Elimu yao, kwani nidhamu itawasaidia katika kufikia malengo yao ya Kitaaluma na Maisha kwa Ujumla.
Ndg. Magaro Ameyasema hayo wakati wa Hafla ya kuwaombea Dua wanafunzi wa Kidato cha sita katika mitihani yao ya taifa inayotarajiwa kuanza tarehe 05/05/2025 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilwa, tarehe 29/04/2025. Hafla hiyo imeudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Halmashauri, Viongozi wa Dini, walimu na wananchi kwa ujumla.
Pia Ndg. Magaro amewapongeza Wataalamu wa Elimu Wilayani humo kwa kuweka utaratibu wa kufanya Dua kwaajili ya Wanafunzi wanaoelekea katika Mitihani ya Mwisho, huu akisisitiza Kuwa hatua hii inasaidia kuwaita Moyo wanafunzi na kuongeza hamasa ya ufaulu katika Shule hizo.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Ndg. Kassim Mpanda amewataka wanafunzi hao kutumia vizuri muda uliobaki katika kujisomea nakujiandaa na Mitihani yao ili kupata matokeo mazuri yatakayowawezesha kuendelea na safari ya kitaaluma.
Kadharika Afisa Elimu Taaluma Ndg. Robert Bujiku amewasisitiza wahitimu hao kuzingatia nidhamu katika kipindi kilichobaki ili kuepuka makosa ya kinidhamu na kuepuka usumbufu wa adhabu za kinidhamu katika kujiandaa na Mitihani iliyoko mbele yao.
Akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya wanafunzi wote, Mwanafunzi mmoja wa kidato cha sita aitwaye Israel Macha amewashukuru walimu, viongozi wa dini na viongozi wa Wilaya na Halmashauri kwa kuendelea na jitihada za kuinua Elimu kuanzia walipojiunga katika Shule hiyo mpaka hatua ya kuwapa Moyo kwa kuwafanyia Dua ya pamoja kuelekea Mitihani yao ya mwisho katika hatua hiyo ya elimu.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa