Ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya Sekondari Ngome wenye thamani ya shilingi milioni95,000,000 imeleta nafuu kwa walimu wa shule hiyo kwa kupunguza gharama za maisha ikilinganishwa na zamani ambapo walilazimika kuishi umbali mrefu na eneo la kazi.
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Mwl. Emanuel makelele anaeleza kuwa kabla ya ujenzi wa nyumba hiyo walikuwa wanapata changamoto ya makazi hususani kipindi cha mvua ambapo hali hiyo ilikuwa inaathiri ufundishaji wao.
Aidha mwalimu Makelele ameishukuru serikali ya awamj ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ambayo imekua mkombozi kwao.
Hata hivyo hakusita kumpongeza Mkurugenzi Mtendeji wa Halmashauri ya Kilwa kwa usimamizi mzuri wamradi huo kwani umejengwa katika uboramaridhawa na kukamilika kwa wakati.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa