UFUTA WA MIL 81 WAKAMATWAUKITOROSHWA KILWA*
Uongozi waHalmashauri ya wilaya Kilwa umefanikiwa kukamata ufuta tani 32 ukiwaunatoroshwa kutoka chama cha Msingi cha ushirika Linali kata ya Likawage wilayaya Kilwa .
Mzigo huoumethibitika ni wa wizi baada ya kamati ya Ulinzi na usalama ukiongozwa na mkuuwa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai kuutilia mashaka haliiliyopelekea uchunguzi kufanyika ili kubaini uhalali wake.
Afisa Ushirika wa Wilaya ya Kilwa ndg Christopher Soka kuthibitisha kuwakampuni ya Hashim and Sons walikuwa wameshamaliza mzigo wao walioununua katikaWilaya ya Kilwa hivyo hawakuwa na bakaa yoyote ya ufuta.
Baada yataarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Christopher Ngubiagai*amwagiza Mkuu wapolisi Wilaya ya Kilwa(OCD) kuukamata mzigo huo na wahusika wote waliohusikakutengeneza nyaraka zisizo halali kukamatwa na kufikishwa mahamani.
*Mhe.Ngubiagai* ametoa onyo Kali kwa vya vya msingi vya ushirika kuacha Maramoja tabia yenye lengo la kuwaibia wananchi ambapo mpaka sasa zaidi ya tani elfu mbili zenye thamani ya zaidi ya 570mil.zimeripotiwa kuibiwa katika maghalambali mbali ndani ya Wilaya ya Kilwa.
Imetolewa na
David Langa
Afisa habari H/W Kilwa
20/08/2019
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa