Kilwa,
Katika kuhakikisha ardhi inawanufaisha wananchi wa wilaya ya Kilwa na taifa kwa jumla.Mkuu wa wilaya hiyo,Christopher Ngubiagai amesema mashamba yaliyotelekezwa na kusababisha mapori wilayani humu yatataifishwa na kugawiwa kwa watu wenye uwezo wa kuyaendeleza.
Ngubiagai ametoa tamko hilo leo katika kijiji cha Marendego alipokuwa anazungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara,uliofanyika kijijini hapo.
Amesema nijambo lisilokubalika kuona baadhi ya wananchi wilayani humu wakiwa hawana maeneo ya kulima,huku baadhi ya wananchi wamehodhi maeneo makubwa na kushindwa kuyaendeleza.Tena yakiwa yametelekezwa kwa miaka mingi na kusababisha mapori ambayo yamegeuka na kuwa hifadhi zisizo rasimi za wanyama waharibifu wa mazao ya kilimo.
Kufuatia hali hiyo,mkuu huyo wawilaya ya Kilwa mkoani Lindi amewataka wananchi waliotelekeza mashamba yao kwa muda mrefu wasafishe haraka na wahakikishe yanakuwa safi kabla ya mwezi Desemba mwaka huu.Kwasababu kuanzia mwezi huo mashamba yatakayo kutwa hayasafishwa yatagawiwa kwa watu wenye huitaji na wanaoweza kuyaendeleza.
Amewataka viongozi na watendaji wa vijiji waanze kuyabaini na kuorodhesha mashamba yaliyotelekezwa kwamuda mrefu ili ifikapo mwezi huo iwe rahisi kuyagawa.Kwasababu yatakuwa yanajulikana yapo wapi na kwamuda gani yamebaki bila kufanyiwa kazi.
Ngubiagai aliwatoa hofu wananchi kwamba zoezi hilo litatendeka kwa haki bila kupendelea na kumuonea mtu.Huku akiwataka viongozi na watendaji kuwa makini na waongozwe na uadilifu, uaminifu na uzalendo.Nayeyote atayeharibu zoezi hilo kwa masilahi binafsi atakuwa anathibitisha kuwa hasitahili kuwa kiongozi.
Mkuu huyo wa wilaya katika kuonesha hajakurupuka kufikia uamuzi huo alisema amebaini kuwa mashamba mengi yaliyotelekezwa yamehodhiwa na watu wanaoishi nje ya wilaya ya Kilwa.Hata wanapoombwa wawape wanaotaka kuendeleza wanakataa.Huku wengine wakiuza kwa bei kubwa ili yasinunuliwe.
"Ukiuliza unaambiwa shamba lilikuwa la babu wa babu yake,mwenyewe anaishi Temeke.Hapa ameliacha nakugeuka pori linalotunza nguruwe.Kama yupo Temeke achukue aishi nalo hukohuko lakini likibaki Kilwa bila kuendeleza nagawa kwawenyehuitaji,"alisema Ngubiagai.
Mbali na onyo hilo, Ngubiagai amewataka wananchi wilayani humu kutoa ushirikiano na kuwathamini watumishi wa serikali na kuacha mara moja tabia ya kuwazuia wasitimize na kutekeleza majukumu yao.Kwani baadhi yao wanatishia usalama wawatumishi wanapotekeleza majukumu yao.
Alitolea mfano tukio lililotokea juzi,kwamba baadhi ya wananchi waliwafurusha na kuwatishia maisha wataalamu wa idara ya ardhi wa halmashauri ya wilaya hiyo ambao walikuwa wanapima mipaka ya vijiji viwili vilivyokwenye mgogoro wa mipaka.Hata hivyo wanachi wakijiji kimoja kati ya hivyo viwili waliwafurusha wataalamu hao nakusababisha washindwe kuendelea na kazi.
"Tabia hiyo naomba ikome,iwe mwanzo na mwisho.Wapeni ushirikiano na msiporidhika na jambo fulani fuateni na kuzingatia sheria.Siyo kuwatishia maisha na kuwazuia kufanya kazi.Hao ni watoto wawenzenu, nibinadamu kama nyinyi,"alisema kwa hasira Ngubiagai.
Wilaya ya Kilwa inahekta takribani 800,000 za ardhi zinazofaa kwa kilimo.Hata hivyo baadhi ya maeneo yamehodhiwa na watu ambao wameshindwa kuyaendeleza.Hali inayosababisha kuwepo mapori na vichaka hata katikatika ya vijiji,miji midogo ya Kivinje na Masoko na pembeni ya barabara kuu.
Credit - Muungwana Blog
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa