Katika kuhakikisha ushiriki wa wananchi katika maendeleo ya jamii , Taasisi ya Tumaini Jipya la Wanawake Kilwa (TUJIWAKI) imewasilisha rasmi Mradi wa Raia Makini kwa uongozi wa Wilaya ya Kilwa, lengo ikiwa na kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya ushiriki wao katika utawala bora na ufuatiliaji kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 31 Julai 2025 katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ambapo waratibu wa mradi huo wameeleza mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 30 kuanzia Januari 2025, katika vijiji vya Nanjirinji A na Miguruwe, huku ukilenga kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika masuala ya uwajibikaji, usimamizi wa rasilimali za umma, na utawala bora.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mratibu wa Mradi, Bi. Pili Makame amesema kuwa mradi huo unalenga kuwawezesha wananchi kuelewa na kushiriki kikamilifu katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, pamoja na kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha utekelezaji wenye tija wa huduma za kijamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mohamed Nyundo, ameipongeza Taasisi ya TUJIWAKI kwa kushiriki katika ujenzi wa jamii bora, hususani kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuelewa utekelezaji wa Serikali, uwajibikaji wa viongozi, na matumizi sahihi ya fedha za umma.
Aidha, Mhe. Nyundo amewataka watekelezaji wa mradi huo kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unafanyika kwa weledi na ufanisi, ili ulete manufaa ya kweli kwa wananchi, huku akihimiza uratibu wa miradi mingine ya maendeleo ambayo inaweza kuendelea kuinufaisha jamii ya Wilaya ya Kilwa.
Mradi huu unatekelezwa juu ya ushrikiano kati ya Taasisi za Wajibu Institute of Public Accountacy pamija na Policy Forum
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa