Sport Development Aid Wamekabidhi vifaa vya michezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndugu Hanan Bafagih ikiwa ni muendelezo wa kusapoti Sekta ya Michezo mashuleni kwa Shule za Sekondari
Afisa wa Mradi wa Sport Development Aid Godwin Malley amesema mradi ambao wanaendelea nao kwa Shule za Sekondari ujulikanao kama Empowering Boys’ Society Through Sport and Health Education ni mradi ambao unalengo la kumsaidia kijana wa kiume katika kutambua nafasi yake katika jamii sambamba na kupinga mfumo dume na pia kumjengea uwezo wa kujitambua.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Hanan Bafagih amewashukuru wadau hawa muhimu katika kuhakikisha wanaunga mkono jitihada za kukuza na kuendeleza michezo katika mashule jambo litakalosaidia kuwalinda vijana na kuwaunganisha na kuwajengea tabia njema hata hivyo amewaomba waangalie jinsi ya kuwasaidia pia wanafunzi wa elimu ya msingi kwa kuwapatia vifaa vya michezo ili nao waweze kujihusisha na michezo kwa sababu michezo ni afya.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri amekabidhi Maafisa Elimu Vifaa hivyo, Mkurugenzi amewaomba watenge muda wa michezo katika shule zote ili wanafunzi waweze kushiriki vizuri michezo kwa sababu michezo ni ajira na itasaidia kuwatengenezea uwezo wa kujitambua na kuwaepusha na tabia zisizofaa katika jamii.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa