Kilwa,
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa imepokea msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni kumi na tano kutoka Kampuni ya Songas.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Julai 18 katika viunga vya halmashauri ya wilaya ya kilwa Meneja mahusiano ya jamii kutoka kampuni ya Songas Bw. Nicodemus Chipakapaka amesema kampuni ya Songas itaendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukishiriki katika kusiadia jamii katika Nyanja tofauti tofauti kama vile elimu, afya na zinginezo.
Leo tumekabidhi Kompyuta, Printa na vifaa vingine ambavyo vina thamani ya Shilingi milioni kumi na tano kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma ya afya na tutaendelea kushirikiana katika mambo mengine kadri tuwezavyo” alisema Chipakapaka.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo (kushoto) akipokea printa kutoka kwa Meneja Mahusiano ya jamii , Kampuni ya Songas Ndg. Nicodemus Chipakapaka katika hafla fupi ya Makabidhiano iliyofanyika Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Picha: Ally Ruambo).
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo ameishukuru kampuni ya songas kwa msaada wa vifaa hivyo na kuahidi kuvitumia vizuri katika kuimarisha mfumo wa taifa wa kuhifadhi taarifa Hospitalini GoTHoMIS katika Hospitali ya Wilaya na kufunga Mfumo wa GoTHoMIS katika kituo cha Afya Masoko ili kuongeza mapato zaidi.
Bugingo amesema kabla ya mfumo wa GoTHoMIS makusanyo katika Hospitali ya Kinyonga yalikua ni kati ya milioni moja mpaka milioni mbili kwa mwezi na baada ya mfumo makusanyo yamepanda mpaka kufikia milioni tisa mpaka kumi kwa mwezi.
“Hospitali ile ya Wilaya ilikua inauwezo wa kukusanya kati ya milioni moja mpaka milioni mbili lakini baada ya kufunga huu mfumo sasa hivi inaweza kujikusanyia kati ya milioni tisa mpaka kumi kwa mwezi, kwa hiyo kwa vifaa hivi vipya tutaenda kuboresha mfumo na tunaimani mapato yataongezeka zaidi pale hospitali na katika kituo cha Afya Masoko ambapo mfumo wa GoTHoMIS unaenda kuanzishwa.
Huu ni mwanzo tu lakini baadaye vituo vyetu vyote vitatumia mfumo huu katika kuendesha shughuli zake za kila siku” alisema Bugingo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Bw. Zablon Bugingo akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kukabidhiwa Vifaa mbalimbali kutoka Kampuni ya Songas katika hafla fupi iliyofanyika Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Picha: Ally Ruambo).
Naye Mganga mkuu wa Wilaya ya Kilwa Dokta. Khalfan ameishukuru Kampuni ya Songas kwa msaada wao na kukaribisha Makampuni na Mashirika mengine kusaidia Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wakiwa katika hafla fupi ya Makabidhiano ya Vifaa kutoka Kampuni ya Songas, Mkabidhiano iliyofanyika Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Picha: Ally Ruambo).
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa