Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Rais- Tamisemi Mhe.David Silinde amewapongeza viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa ujenzi wa madarasa bora na kwa wakati.Mhe.Silinde ameyasema hayo katika siku yake ya kwanza ya Ziara ya siku nne katika mkoa wa Lindi .Mhe.Silinde alianza ziara yake katika shule ya sekondari Mingumbi ambapo alikagua ujenzi wa madarasa mawili yaliyojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R na darasa moja lililojengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri .Baadaye Mhe.Silinde alitembelea shule ya sekondari Kivinje ambapo madarasa matano yamejengwa kwa fedha za ndani kwa thamani ya sh.milioni 75 ambapo madarasa yote yamekamilika na yameanza kutumika.Mhe.Silinde pia alitembelea kikundi cha vijana cha Kivinje Jogging Club kinachojishughulisha na uzoaji wa taka kwa kutumia gari lenye thamani ya shilingi milioni 18 walilokopeshwa na halmashauri ikiwa ni sehemu ya mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa vijana ,wanawake na walemavu ambapo aliwapongeza na kuwataka wabuni miradi mingine zaidi ili kuweza kujiongezea kipato.Halmashauri ya wilaya ya Kilwa ilikuwa na upungufu wa madarasa saba kwa ajili ya wanafunzi ya kidato cha kwanza ambapo mpaka sasa halmashauri imetumia zaidi ya milioni 105 kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa hayo katika shule za Ally Mchumo, Kikanda ,Kivinje ,Dodomezi na Namayuni.Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya kilwa Bw.Renatus Mchau amemuhakikishia Mhe.Silinde kuwa mpaka sasa halmashauri yake haina upungufu wa madarasa kwa shule za sekondari.Baada ya kufanya majumuhisho ya ziara Hiyo ya siku moja ,mhe.Silinde ameelekea Wilaya ya Liwale ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne .David LangaAfisa Habari16/02/2021
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa