Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Hospital ya Oceani Road wakitimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan imetembelea Ofisi ya za Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa na kuzungumza na Viongozi pamoja na Watumishi wa Halmashauri hiyo, kuhusiana zoezi la utoaji wa Huduma ya Uchunguzi na Matibabu ya Magonjwa ya Saratani kwa Wananchi wa Wilaya ya Kilwa katika Hospital ya Wilaya (Kinyonga).
Huduma hizo Zitazotolewa bure kwa siku Tatu kuanzia leo tarehe 28 hadi 30/04/2025 lengo kuu la kutoa huduma hizo ni kutoa matibabu kwa wananchi na kuikomboa jamii kutokana na magonjwa ya Saratani kama vile Saratani ya Mlango wa Kizazi, Saratani ya Tezi Dume, Saratani ya Ngozi na nyinginezo.
Akizungumza na Madaktari hao Katibu Tawala wa Halmashauri ya Kilwa Ndg.Yusuf Mwinyi ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuelekeza Msaada huo wa Kiafya kwa Wananchi wenye uhitaji,kwani hii itaenda kusaidia jamii kupata huduma za matibabu ya Kibingwa bure, pia kupata Rufaa ya moja kwa moja katika Hospiatali zenye Madaktari bingwa wa Magonjwa ya Saratani ukitofautisha na hapo mwanzo.
Pia Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Hemedi Magaro amewapongeza Madaktari hao kwa Ujio wao kwaajiri ya kutoa huduma kwa wananchi wa Wilaya ya Kilwa, huku akitoa wito kwa watumishi na Wananchi wa Wilaya hiyo kutumia Fursa hiyo ili kujua hali zao za Afya bila Malipo katika Hospitali ya Wilaya, aidha amesema wao kama Viongozi jamii hiyo wapo tayari kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa Zoezi hilo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa