Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP John M. Imori amefanya kikao kazi na Viongozi wa Vyama vya Siasa Wilaya ya Kilwa, ikiwa ni hatua ya kuelimishana na kukumbushana haki na wajibu wa Vyama vya Siasa pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Uchaguzi. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Kilwa leo tarehe 30 Oktoba 2024.
Katika kikao hicho Kamanda Imori amewasisitiza Viongozi wa Vyama vya Siasa kujiepusha na utoaji wa kauli za uchonganishi, uvunjivu wa sheria na kuvuruga Amani katika kipindi cha Kampeni za uchaguzi badala yake amewataka kutumia muda wao kunadi na kutangaza sera zao kwa wananchi. "Kila mwenye wajibu na atimize wajibu wake, Tukiepuka vurugu hatutakutana"
Amesema Kamanda Imori.
Naye Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro ametoa wito kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa kuendelea kutoa ushirikiano kwa wasimamizi na Wadau wa Uchaguzi, Pia kutoa taarifa kuhusiana na changamoto zinazojitokeza mapema iwezekanavyo ili ziweze kutatuliwa.
Kwa upande wao Viongozi wa Vyama vya Siasa wameomba Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Wasimamizi wa Uchaguzi kutimiza wajibu wao kwa kufuata miongo na taratibu zinazosimamia Uchaguzi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa