RC.Zambi asisitiza uadilifu, uwajibikaji kwa watumishi wa umma
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Godfrey Zambi anaendelea na ziara ya kikazi ya siku tano katika Wilaya ya Kilwa. Katika siku ya kwanza ya ziara Mhe Zambi alikagua miradi ya maendeleo, kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuongea na watumishi katika kata ya Kipatimo.
Katika kata ya Somanga, Mhe.Mkuu wa Mkoa alikagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Somanga ambacho kilianza kwa nguvu za wananchi na sasa kimepata ufadhili kutoka kampuni ya uchimbaji gesi ya Pan Africa Energy Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni mia nane(800 milioni).
Katika siku ya pili ya ziara ya Mhe.Mkuu wa mkoa alitembembea tarafa ya Pande na kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Pande kinachojengwa kwa utaratibu wa maboresho ya sekta ya Afya inayosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo kituo hicho kilipokea shilingi milioni mia nne na mpaka sasa ujenzi umefika asilimia 85 katika hatua ya umaliziaji.
Siku ya tatu ya ziara ya Mkuu wa Mkoa akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Christopher Ngubiagai, kamati ya Ulinzi na usalama, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya a Kilwa Ndg Renatus Mchau, wakuu wa Idara na Vitengo , Mhe.Mkuu wa Mkoa alianza ziara katika Kata ya Tingi kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Tingi kinachojengwa kwa thamani ya shilingi Milioni mia nne(400milioni) toka ofisi ya Rais Tamisemi. Akiwa katika kituo cha Afya-Tingi, Mkuu wa mkoa alioneshwa kuridhishwa na ujenzi lakini akasisitiza hatua iliyofikiwa kukamilishwa kabla ya mwezi wa Julai mwaka huu ili majengo hayo yaanze kutumika.
Baada ya hapo Mkuu wa Mkoa alipata nafasi ya kuongea na watumishi wa Halmashauri katika ukumbi wa Chuo cha Maendeo Kilwa ambapo alisisitiza uwajibikaji wa watumishi katika kuwatumikia wananchi, sisi ni watumishi wa umma, lakini wajibu wetu mkubwa ni kuwatumikia wananchi, tuwatumikie bila kubagua na bila kuomba rushwa ili tutoe huduma’’ aliongeza Mhe.Zambi. Mhe.Zambi aliongeza kuwa kila mtumishi ajue dhamana aliyokabidhiwa katika serikali na kuhakikisha malengo ya serikali ya awamu ya tano ya Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli yanafikiwa.
Kesho tarehe 22 Mhe.Zambi ataendelea na ziara katika Wilaya ya Kilwa…..
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa