Mkuu wa mkoa Lindi Mhe. Zainab Telack amewapongeza maafisa kilimo pamoja na maafisa Ushirika kwa kusimamia kilimo mkoani humo.
Pongezi hizo amezitoa leo Julai 2,2025 kwenye kikao Cha wadau wa korosho kikiwa na lengo la kujadili zao hilo Kwa Mkoa wa Lindi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Aidha amewaomba maafisa kilimo kuendelea kutoa Elimu na kushawishi Vijana kuweza kujiajiri kwenye sekta ya kilimo Kwani Mkoa wa Lindi una maeneo mengi mazuri kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Sambamba na hilo RC Telack ametoa rai kwa wakulima kuwatumia maafisa kilimo ili kuepukana na magonjwa ya mikorosho ambayo yanaweza kusababisha kupata mazao yasiyo bora.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania Bw, Francis Alfred amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuwapatia wakulima pembejeo za Bure ambazo kwa kiasi kikubwa zimepelekea kuongeza Uzalishaji wa zao la korosho na kusaidia kuboresha maisha ya wakulima wengi Kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa