Kilwa,
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akisalimiana na watumishi mbalimbali kutoka idara ya Afya baada ya kuwasili katika viwanja vya Garden Mkapa mjini Kilwa Masoko tayari kwa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani (Picha na Ally Ruambo).
Wananchi Wilayani Kilwa wametakiwa kuithamini na kuilinda amani ya nchi kwa hali na mali.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi April 26 alipokua akihitimisha maadhimisho ya siku ya Malaria duniani iliyoadhimishwa ki Mkoa Wilayani Kilwa katika viunga vya Garden Mkapa.
Zambi emesema kuna Watu ambao wamekuwa hawaitakii mema Tanzania, wanataka kuivunja misingi imara ya upendo na Amani iliyowekwa na waasisi wa Taifa Mwalimu Julias Nyerere na mzee Abeid Karume.
“Kuna watu wanataka kuvunja amani ya nchi hii iliyowekwa na waasisi wetu Mwalimu Julias Nyerere na Mzee Abeid Karume naomba tusikubaliane nao, kuna maeneo Watu hawezi kukutana kama jinsi tulivyokutana sisi hapa leo kutokanna na amani kutoweka.
Nikiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa niwahakikishie kwamba tutawashughulikia wale wote ambao kwa namna moja au nyingine watajaribu kuvunja amani tuliyo nayo” alisema Zambi.
Adha, amewataka wananchi kuzipuuzia imani potofu zinazosambazwa na watu juu ya matumizi ya vyandarua kwani hazina ukweli wowote.
“Kuna watu wanasenma kwamba akitumia chandarua, akiwa amelala anaona kama yupo kwenye Jeneza, sasa hata kama unaogopa Jeneza kwani kuna ambaye hatokufa? Wengine wanasema ooh zinapunguza nguvu za kiume, ni uzushi huu ndugu wananchi naomba tuupuze na tutumie vyandarua kwa ajiri ya kujikinga na Mbu waenezao Malaria” alisisitiza Zambi.
Pia amewataka Wananchi kufuata maelekezo ya Wataalumu juu ya kujikinga na Malaria ikiwemo kuangamiza kabisa mazalia ya Mbu kwa kufukia madimbwi ya maji machafu, kufyeka Vichaka kuzunguka makazi na njia nyinginezo.
Awali akitoa salamu za wilaya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai ameshukuru kwa Wilaya ya Kilwa kupewa Hadhi ya kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ki Mkoa na kuwataka Wananchi kujikinga na Malaria kwa kufanya usafi wa mazingira , kuangamiza mazalia ya Mbu na kutumia Vyandarua ipasavyo.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani Mkoa wa Lindi yaliyofanyitika Wilayani Kilwa Mhe. Godfrey Zambi akipata maelezo ya jinsi Malaria inavyozuiwa alipotembelea moja wapo ya mabanda yaliyoshiriki katika maonyesho ya siku ya Malaria Duniani (Picha na Ally Ruambo).
Kila ifikapo April 25 Dunia uadhimisha siku ya Malaria duniani kwa kukutana na kujadili mafanikio na na changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha jitihada za kumaliza tatizo la Malaria na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kutoa elimu ya kina juu ya madhara na jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo hatari.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa