Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Mkono wa Eid kwa watoto wenye mahitaji Maalum Shule ya Msingi Mtanga Wilayani Kilwa.
Mhe. Rais ametoa Salamu hizo kupitia Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack Ambae amewakilishwa na Kaimu MKurugenzi Ndg. Shija Lyella ambazo zimewasilishwa katika Shule ya Msingi ya watoto wenye mahitaji Maalumu Mtanga iliyopo halmashauri ya Kilwa Mkoani Lindi.
Ndg. Shija Lyella akiwasilisha salamu hizo, amewasihii wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kufikia ndoto zao huku akitoa wito kwa walimu na wazazi kuhakikisha watoto hao wanasimamiwa vema kwani serikali imefanyakazi kubwa yakuhakikisha inajenga na kuweka miundombinu wezeshi kwa wanafunzi wenye uhitaji nchi nzima ikiwemo Mkoa wa Lindi, hivyo jukumu la wazazi, walezi na walimu kuwapa ushirikiano watoto ili wafikie ndoto zao .
Akitoa Shukrani kwaniaba ya watoto na uongozi wa shule, Omari Naise Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, anamshukuru Mhe. Rais na uongozi wa Mkoa na Halmashauri ya wilaya ya kilwa kwakuwakumbuka mara kwa mara na kuahidi kuendelea kufanyakazi kwa ushirikiano na upendo mkubwa kwa wanafunzi hao wenye uhitaji.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa