Shirika la Upendo Youth Development Organization (UYODEO) limewasilisha Mradi wa Raia Makini kwa uongozi wa Wilaya ya Kilwa, lengo ikiwa ni kuongeza ushiriki wa wananchi katika uwajibikaji, matumizi ya rasilimali za umma na utawala bora.
Kikao hicho kimefanyika Tarehe 28 Julai, 2025 katika Ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ambapo wawakilishi wa UYODEO wameeleza kuwa mradi huo ulioanza tangu Januari 2025 katika Kata za Njinjo na Nanjirinji, Vijiji vya Nakiu na Kipindimbi.
Akizungumza afisa miradi UYODEO Ndg.Amani Kiwaula amesema mradi huo unalenga kutoa elimu na kuwawezesha wananchi juu ya kufuatilia miradi ya maendeleo na kushirikiana na viongozi kusimamia matumizi ya fedha za umma.
Nae Mkurugenzi wa UYODEO Ndg.Sylevester karigita ameongeza kuwa Matarajio ya mradi ni kuongezeka kwa ushiriki wa wananchi katika vikao vya maendeleo, kuimarika kwa uwazi, na mawasiliano bora kati ya jamii na viongozi.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Wilaya Ndg. Yusuf Mwinyi amewataka wawakilishi wa UYODEO kuhakikisha suala la uwajibikaji na kujitoa kikamilifu katika utekelezaji wa mradi, huku akisisitiza kuwa mafanikio yanatokana na utekelezaji wa vitendo vinavyoleta mabadiliko kwa wananchi.
Mradi huu wa Raia Makini unatekelezwa kwa ushirikiano na Taasisi za Wajibu institute of public accountability na policy forum Ukiwa umefadhiliwa na EU (Uropean union)
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa