• Malalamiko |
    • Anuani Zetu |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Kilwa District Council
Kilwa District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Mikakati ya Halmashauri
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Afya
      • Utumishi na Utawala
      • Elimu ya Msingi
      • Mipango na Takwimu
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Fedha na Biashara
      • Maliasili
    • Vitengo
      • Usafi na Mazingira
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • TEHAMA
      • Nyuki
      • Biashara
      • TASAF
      • Lishe
      • Uvuvi
    • Miji Midogo
      • Masoko
      • Kivinje
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Huduma za Uwekezaji
    • Biashara na Viwanda
    • Madini
    • Uvuvi
    • Utalii
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Mikopo kina Mama na Vijana
    • Huduma za Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Itakayo tekelezwa
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Mifumo
    • PlanRep
    • FFARS
    • Prem
    • Salary Slip Portal

NEC YATOA VIBALI VYA ELIMU YA MPIGA KURA NA WATAZAMAJI WA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA 23.

Posted on: February 23rd, 2024

NEC YATOA VIBALI VYA ELIMU YA MPIGA KURA NA WATAZAMAJI WA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATA 23.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha tarehe 24 Februari, 2024, kilichofanyika katika Ofisi za Tume Jijini Dodoma imetoa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura wakati wa uchaguzi mdogo wa Udiwani katika kata 23 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 20 Machi, 2024 kwa asasi za kiraia 11.

Kwa Mujibu wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Kailima, R. K imeainisha Asasi za kiraia 11 ambazo zimekidhi vigezo na kupewa vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura pamoja na kata walizoomba kutoa elimu  hiyo kuwa ni Mbogwe Legal Aid Organization (MBOLAO) Isebya iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe, Sustainable Hub for Policy Initiatives (SHPI) Mshikamano iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.

Asasi zingine ni Promotion and Women Development Association (PWDA) Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Bagamoyo Community Capacity Empowerment and Education (BCCEE) Fukayosi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Action for Democratic Governance (A4DG) Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.

Asasi zingine ni Vanessa Foundation ambayo itatoa elimu katika kata ya Nkokwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Tanzania Centre for Disability Development Initiatives (TCDDI) Nkokwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Safe Society Platform Tanzania (SSPT) Busegwe iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama na Isebya iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe

Asasi zingine za kiraia zilizopata kibali ni Youth Against Aids and Poverty Association (YAAPA) ambayo itatoa elmu katika kata ya Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Musoma Municipal Paralegal Organisation (MMPO) Mshikamano iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.

Asasi nyingine iliyopata kibali ni Shirika la Elimu ya Uraia na Uzalendo “Civic Education and Patriotism Association” iliyoomba kutoa Elimu katika kata za Kimbiji iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Msangani iliyopo katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Fukayosi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlanzi iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Kibata iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Wakati huo huo, Tume pia imetoa kibali kwa asasi za kiraia tatu ambazo zimekidhi vigezo ili ziweze kutazama uchaguzi mdogo wa Udiwani katika Kata 23 za Tanzania Bara.

Asasi hizo tatu zitakazoenda kutazama uchaguzi Mdogo wa udiwani siku ya Jumatano tarehe 20 Machi, 2024 ni Tanzania Alliance for Disability Development Initiatives itakayokuwa katika kata ya Mhande iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Bridge Development Trust Organisation itakuwa katika kata ya Buzilasoga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Promotion and Women Development Association itayokuwa katika Kata ya Kasingirima iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Aidha, katika kikao hicho, Tume imezitaka asasi za kiraia zilizopata kibali cha kutoa elimu ya mpiga kura, kuzingatia Mwongozo wa Elimu ya Mpiga Kura wa Mwaka 2020 katika kipindi chote cha kutoa elimu hiyo  katika uchaguzi mdogo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI HALMASHAURI YA WILAYA YA KILWA September 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 04, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KILWA DC YAANZA KWA KISHINDO SHIMISEMITA

    August 16, 2025
  • MTANDAO WA BMU WAELEZA FAIDA ZA ZIARA YA MAFUNZO MKOANI TANGA

    August 15, 2025
  • DED NA TIMU YA UFUATILIAJI KILWA WAFANYA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO

    August 14, 2025
  • KAMATI ZA MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MAJIMAJI KILWA ZAKUTANA KUJADILI MAANDALIZI YA SHEREHE HIZO

    August 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Akipokea Mwenge wa Uhuru.
Video Zaidi

Kurasa za Haraka

  • TARURA GPN
  • Watumishi Portal
  • MIKOPO 10%
  • Mikopo ya Wanawake na Vijana
  • Huduma za Elimu

Tovuti Muhimu

  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ikulu
  • Wizara ya Fedha
  • Wizara ya Elimu
  • Lindi

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani ya Mahali

Anuani Zetu

    Kilwa Masoko

    Anuani ya Posta: 160

    Simu: 0672365354

    Simu: 0672581557

    Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Kanuni Binafsi
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa