Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Mhe. Farida Kikoleka, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii Wilayani humo, Kutoa Mikopo kwa Vikundi vya watu wenye sifa ili kukomesha tabia ya wakopaji wasiofanya marejesho ya mikopo hiyo.
Mhe.Kikoleka ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango kilichofanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii (FDC) Kilwa leo Tarehe 30/12/2024.
Aidha Mhe. Kikoleka Ametoa pongezi kwa wataalam hao kwa kuwapatia wananchi elimu juu ya faida za mikopo isiyo na riba inayotolewa na Halmashauri pia kuwahamasisha wananchi hao kuomba mikopo kwa ajili ya kufanya miradi ya maendeleo, hii imepelekea mwitikio mzuri wa uombaji wa mikopo hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Mhe. Ally Mohamed Kasinge ametoa rai kwa Wataalam pamoja na Wanasiasa katika Kamati hiyo kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa majukumu ili kuleta maendeleo kwa wananchi Wilayani Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa