Mwenge wa Uhuru 2025 umetembelea mradi wa ujenzi wa Zahanati mpya ya kijiji cha Njinjo na kuona ujenzi wa Zahanati hiyo inayojengwa kwa nguvu za wananchi, Mapato ya Ndani, Wadau wa Maendeleo na Serikali kuu ambao umepangwa kutekelezwa kwa awamu mbili kwa gharama ya Tsh Milioni 327,093,000/=
Akiwasilisha taarifa ya mradi mbele ya kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Dkt. Fredrick Moshi, Mganga Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kukamilika kwa mradi huu utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwa kupata huduma za Afya karibu na makazi yao na kupunguza uwezekano wa kutokea vifo vya wajawazito na watoto wachanga.
Ndugu Ismail Ali Ussi kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025 amewapongeza wananchi wa Njinjo kwa kudhubutu kuibua miradi kama hiyo ya afya ambapo Mhe. Rais anaungana na wananchi kwa kutoa fedha za miundombinu, watumishi na vifaa tiba.
Mara baada ya kutembelea mradi huo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru ameridhia kuweka Jiwe la Msingi na kupongeza jitihada za serikali katika utekelezaji wa majukumu ya kuwahudumia wananchi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa