Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025 Comredi Ismail Ali Ussi ameongoza Mbio za Mwenge wa uhuru zenye umbali wa kilometa 173 wilayani Kilwa tarehe 31 Mei, 2025 ili kutembelea miradi 13 kwa ajili ya kuona, kuweka mawe ya msingi na kufanya Uzinduzi katika miradi hiyo ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya Tsh Bilioni 11,620,849,442/= kuashiria uchochezi wa Maendeleo Wilayani Kilwa.
Katika mbio hizo Mwenge wa Uhuru umetembelea na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili (2) ambayo ni Mnada wa Mifugo ulioko katika Kata ya Njinjo wenye thamani ya Tsh 74,020,410/= ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Njinjo wenye thamani ya Tsh 327,093,000/=. Pia mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa madarasa mawili (2) katika shule ya Msingi Matandu wenye thamani ya 48,000,000/= lengo ikiwa ni kuboresha ustawi wa wananchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Pia Mwenge wa Uhuru umetembelea na kuona mradi wa Uhifadhi wa Mazingira katika Msitu wa Kijiji cha Ngea katika Kata ya Mitole na Kupanda miti kama ishara ya kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira, Pia Mwenge wa Uhuru umetembelea na kuona mradi wa duka la uuzaji wa vifaa vya ujenzi unaomilikiwa na Vijana wanufaika wa mikopo ya Asilimia 10% kutoka Halmashauri wenye thamani Ths. 45,000,000/=
Samabamba na hayo Mwenge wa Uhuru umetembela na kuona hali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja la Mikereng’ende katika kata ya Tingi wenye thamani ya Sh. 11,116,536,032/= Aidha Mwenge wa Uhuru umetembela na kuona Shughuli za mapambano dhidi ya UKIMWI, Rushwa, Malaria, Madawa ya Kulevya na Lishe. Pia Mwenge umetembelea na kuona shughuli za utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura na Matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
Kiongozi wa Mbio hizo ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Wilaya na watendaji wote kwa kwa juhudi zinazofanyika ila kutatua kero za wananchi na kuleta maendeleo wilayai Kilwa. Aidha Amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia kutoa fedha za miradi ya maendeleo ili kutatua kero za wananchi Wilayani Kilwa
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa