Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemedi Said Magaro ametoa semina kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi juu ya kanuni na maelekezo yanayoongoza uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 leo tarehe 30 Septemba 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kilwa, Kilwa Masoko.
Katika semina hii jumla ya wasimamizi wasaidizi 113 kutoka katika kata 23, vijiji 90 na miji midogo 2 wamekula kiapo cha uaminifu na kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Alice M. Mkasela, Kisha kupewa elimu juu ya kanuni zitakazo waongoza kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024
Aidha msimazi wa uchaguzi amewasisitiza wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuwahimiza wananchi katika maeneo yao kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura utakaofanyika kuanzia tarehe 11hadi 20 Octoba 2024 na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa tarehe 27 Novemba 2024.
"Serikali za mitaa, sauti ya wananchi, jitokeze kushiriki uchaguzi.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa