Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mobhare Matinyi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwatumia Maafisa habari wao kwa ufasaha kwa lengo la kutangaza Miradi na shughuli zote zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita.
Matinyi ameyasema hayo alipokuwa leo Tarehe 18/12/2023 katika Mkutano wa Idara ya Habari- Maelezo uliofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambapo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo akiwemo Mkuu wa mkoa Zainab Telack, Katibu Tawala Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa huo, Waandishi wa Habari na Maafisa wa habari wa serikali aidha amesema kuwa lengo la Mkutano huo ni kuwaeleza Wananchi wa Lindi na Watanzania kwa ujumla mafanikio yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wakurugenzi wa Halmashauri zao
hivyo amewataka Wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao kwani inapambana kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazowakabili Wananchi wake.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa