Kuelekea Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba 2024. Msimazi wa Uchaguzi Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro ameongoza kikao baina ya Afisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa Nchini Ngd. Jihadhari Mwinshehe na Viongozi wa Vyama vya Siasa Wilayani Kilwa. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya kilwa tarehe 27 Oktoba 2024.
Lengo la kikao hicho ni kuwakumbusha Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu kanuni na sheria zinazotakiwa kufuatwa wakati wa Uchaguzi, Kuhamasisha Amani wakati wa uchaguzi kwa kuwahimiza Viongozi wa Vyama vya Siasa kufanya kampeni kwa njia ya Amani na kuepuka uchochezi wa vurugu au maneno ya chuki, Pia kuhakikisa Vyama vyote vinapata taarifa sahihi kuhusu taratibu za uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa