MKUU WA WILAYA YA KILWA MHE.CHRISTOPHER NGUBIAGAI AMEKABIDHI PIKIPIKI 59 KWA MAAFISA KILIMO.
Leo Tarehe 22/03/2023 Akikabidhi pikipiki 59 zilizotolewa kwa Maafisa wote Kilimo wa wilaya ya kilwa, Mhe. Christopher Ngubiagai amewataka Maafisa Kilimo kuzitumia pikipiki hizo kwa shughuli ya kuihudumia jamii na si vyinginevyo. Amesisitiza kuwa upatikanaji wa pikipiki hizo uendane na matokeo chanya kwenye sekta ya Kilimo.
amewaasa pia Maafisa hao kutumia pikipiki hizo kwa umakini na tahadhali ili kujilinda na ajali ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya wataalam wa Serikali.
kwani malengo ya serikali ni kuwawezesha Maafisa kilimo kutoa huduma na kuwafikia wakulima wote na kwa wakati sahii , ili kuongeza hali ya uzalishaji na mapato kwa ujumla.
Pia amewataka Maafisa kilimo kuhamasisha wakulima kulima mazao ya muda mfupi kwa kipindi hiki ambacho mvua imekuwa ni changamoto.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa