Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe. Mohamed Nyundo ametoa pongezi kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kwa utekelezaji mzuri wa Majukumu yao. Mhe. Nyundo ameyaeleza hayo wakati wa ufunguzi wa Hafla ya Usiku ya Kilwa Day Festival iliyofanyika Februari 08, 2025 katika Viwanja vya Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa. Lengo la Hafla hiyo ni Kuuaga Mwaka 2024 na Kuukaribisha Mwaka 2025.
Aidha, hafla hiyo ililenga kujenga utamaduni wa kushirikia baina ya Watumishi wa Halmashauri na Wadau, Taasisi, Jamii, na Mashirika Binafsi yaliyoko katika Wilaya ya Kilwa. Katika Hafla hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imetoa Vyeti vya Shukrani kwa Taasisi, Mashirika na Wadau mbalimbali wanaoshirikiana nao katika utekelezaji wa shughuli za Halmashauri kama alama ya kutambua mchango wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed Said Magaro, amewataka watumishi wa Umma kuwa na desturi ya kuhakikisha wanaacha alama zenye manufaa kwa Taasisi na Jamii wanazofanyia kazi. kumbukwe Kilwa Day Festival ilianza na Bonanza la Michezo Asubuhi kisha kuhitimishwa na Hafla fupi jioni.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa