Kilwa,
Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura wametakiwa kutekeleza majukumu waliyopangiwa kwa uweledi wa hali ya juu na kuachana na ushabiki wa Vyama wasimamiapo zoezi la upigaji kura.
Wito huo umetolewa leo Disemba 2 na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Athumani Kihamia alipokuwa akizungumza na wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura katika mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa Chuo cha maendeleo Mjini Kilwa Masoko.
Dk. Kihamia amesema msimamizi hakatazwi kuwa mwanachama wa Chama chochota cha siasa nchini ila haruhusiwi kuleta itikadi pindi anapokuwa anatekeleza majukumu yake ya usimammizi wa zoezi la upigaji kura.
Pia amewataka wasimamizi kuheshimu viapo walivyo apa vya kutunza siri kuanzia kwenye mafunzo, uchaguzi na baada ya uchaguzi kumalizika.
“Naimani kubwa sana na ninyi naimani mpaka kufika hapa mmechujwa vya kutosha na viongozi wenu akiwemo msimamizi wa uchaguzi na timu yake na akaona hawa wanafaa kwenda kusimamia uchaguzi sasa mnatakiwa kuonyesha kile walicho amua kinafanana na ukweli” alisema Kihamia
Wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura wakiwa katika mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa Chuo cha maendeleo Mjini Kilwa Masoko .
Aidha Dk. Kihamia amesema tume imejipanga kuhakikisha hakuna kifaa kitakacho kosekana katika vituo vya kupigia kura na kuahidi ulinzi na usalama vituoni na mitaani wakati wote wa zoezi la upigaji kura.
“Vifaa vyote vitakuwepo kuanzia saa moja asubuhi ambapo vituo vitafunguliwa hadi saa kumi jioni vituo vitakavyokuwa vinafungw , Baadae viongozi wenu hapa watawaeleza juu wa ulinzi lakini Askari watakuwepo vituoni kwa ajili ya kulinda amani lakini pia kutakuwa na patrol katika kata zote za uchaguzi kwahiyo kama mtu ana nia ovu atadhibitiwa mara moja msiwe na wasiwasi kafanyeni kazi kwa mujibu wa maelekezo” alisisitiza Kihamia
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau amewataka wasimamizi kuzingatia mafunzo wanayopatiwa na heshima miongoni mwa wasimamizi na wanainchi wanaoenda kuwasimamia.
Jumla ya Kata nne kutoka katika majimbo ya Kilwa Kusini na Kaskazini zinaenda kufanya uchaguzi mdogo Disemba 2 Mwaka huu kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mitole Mheshimiwa Mnyamba pamoja na waliokuwa Madiwani wa Kata ya Miteja, Somanga, pamoja na Kivinje kwa tiketi ya Chama cha wanainchi CUF kujiudhuru nafasi zao na kuhamia chama cha Mapinduizi kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dokta John Pombe Magufuli.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa