Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ametoa pongezi na shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kuwasogezea Wananchi huduma zote za kijamii kwa ajili ya Maendeleo yao
Ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ya wilaya ya Kilwa katika Mkutano wa Waandishi wa Habari ulliohudhuriwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi pamoja na Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa mkoa huo na kusema kuwa Serikali imeelekeza bajeti yake katika ujenzi na ukarabati katika sekta zote za kijamii ikiwemo Maji, Elimu, Afya, Barabara, Kilimo pamoja na Uvuvi
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa