Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro, ameonyesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Kilwa, ambapo amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia kuleta maendeleo Wilayani Kilwa, Ziara hiyo imefanyika tarehe 28/02/2025.
Miongoni mwa Miradi iliyokaguliwa ni mradi wa Ujenzi wa Mabweni 2, Madarasa 4 na Matundu ya Vyoo 6 katika Shule ya Sekondari Mtanga wenye Thamani ya Tsh. 362,000,000/= Fedha kutoka Serikali Kuu, Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 na Matundu 6 ya vyoo katika Shule ya Msingi Ukombozi wenye Tsh. 83,000,000/= Fedha kutoka Serikali kuu.
Sambamba na hiyo Ndg. Magaro amekagua mradi wa ujenzi wa (vyumba 4 vya madarasa na matundu 2 ya vyoo) wa Shule mpya ya Msingi katika eneo la Mihina wenye thamani ya Tsh 100,000,000/= Fedha kutoka mapato ya Ndani ya Halmashauri. Hiyo yote ni hatua ya kuboresha Mazingira ya upatikanaji wa Elimu Bora kwa Wanafunzi Wilayani Kilwa.
Aidha Ndg. Magaro amewapongeza wasimamizi wa miradi pamoja na mafundi kwa kasi waliyonayo katika kutekeleza miradi hiyo, Pia amesisitiza kuzingatia ubora wa miradi, thamni ya fedha na uaminifu katika kutumia fedha za umma.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa