Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Hemed S. Magaro, ameonyesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Elimu katika Wilaya ya Kilwa ,ambapo amesema Miradi hiyo itasaidia kuinua Elimu Wilayani Kilwa, akiwa katika Ziara hiyo iliyofanyika 8 Desema 2025 Ndg. Magaro Amekagua Miradi mbalimbali ambapo amesisitiza utekelezaji wa haraka wa Miradi hiyo kwa wakati na Ubora unaohitajika.
Miongoni mwa Miradi aliyoikagua ni Ujenzi katika Shule ya Sekondari Mtanga ambapo ujenzi umegharimu Fedha yenye Thamani ya Shilingi Milioni 362 Fedha kutoka Serikali Kuu kwa Mabweni 2, Madarasa 4 na Matundu ya Vyoo 6 katika Shule za Sekondari Mtanga, Shule ya Sekondari Namatungutungu kwa Thamani ya shilingi Milioni 95, kwa Ujenzi wa Nyumba 1 ya Mwalimu (Two in One) Fedha kutoka Mapato ya Serikali kuu, Sekondari Somanga Ujenzi yaliyo gharimu Shilingi Milioni 72 kutoka Mapato ya Ndani na Mfuko wa Elimu,Hiyo yote ikiwa ni hatua ya kuboreshwa Mazingira ya upatikanaji wa Elimu Bora kwa Wanafunzi Wilayani Kilwa.
Aidha Ndg. Magaro pia amekagua Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika maeneo ya Mtondo Kimwaga, ambayo inajengwa kwa Thamani ya Shilingi Milioni 560 Fedha kutoka Mapato ya Serikali kuu kwa Ujenzi wa Madarasa 8,Jengo la Utawala 1,Maabara za kisasa 3,Jengo la Tehama 1,Maktaba 1, Matundu ya Vyoo 10, Tanki la Ardhini na kichomea Taka 1 ambapo Ujenzi wa Shule hiyo unatarajiwa kusaidia kutatua changamoto ya Elimu kwa watoto na kuongeza Ubora wa Elimu.
Sambamba na hilo Ndug. Magaro amempongeza Mkandarasi na msimamizi wa Mradi huo kwa kasi ya Ujenzi wa shule hiyo na amewataka kuongeza kasi Zaidi ili kuhakikisha Ujenzi wa Shule hiyo unakamilika kwa wakati.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa