Kilwa,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Ndg. Renatus Mchau amewatahadharisha watumishi dhidi ya Watu wanaojitambulisha kuwa ni Watumishi kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
Mchau amesema siku za hivi karibuni kuwekuwepo na Watu wasiojulikana wakijitambulisha kuwa ni watumishi kutoka Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na kuwaeleza Watumishi kwa njia ya Simu kuwa taarifa zao za kitumishi sio sahihi na zinaweza kuharibu utumishi wao na kuwataka kutoa kiasi cha pesa na Nyaraka mbalimbali za kiutumishi kama vile cheti cha kuzaliwa, Cheti cha Darasa la saba, kitambulisho cha uraia na vinginevyo kwa ajili ya kuwasaidia kusahihisha taaraifa hizo na kunusuru ajira zao.
Mchau amesema watu hao ni matapeli na ofisi haiwatambui na kuwataka watumishi wasikubali kutoa vielelezo vyao na taarifa zao kwa mtu yeyote bila kuwasiliana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.
“Napenda kuwataarifu watumishi wote kuwa wasikubali kutoa vielelezo au taarifa zozote kwa mtu yeyote bila kuwasiliana na na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kwani watu hao ni Matapeli na Ofisi haiwatambui” alionya Mchau.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa