Kilwa,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kliwa Ngd. Renatus mchau amewaongoza watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, taasisi mbalimbali za kiserikali na wananchi kufanya usafi katika viunga mbali mbali vya Mji wa kilwa masoko.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Mkuu wa kitengo cha Usafi na Mazingira Halmashauri ya wilaya ya kilwa Ndg. Tumaini Kagina amesema ni jukumu la kila Mwananchi kuyatunza na kufanya usafi wa mazingira yanayo mzunguka ili kuepukana na athari mbalimbali zinazotokana na uchafu.
Kagina amesema zoezi la kufanya usafi ni endelevu na amewataka watumishi na wananchi kujitokeza kwa wingi wakiwa na vifaa pindi wanapoenda kufanya usafi.
Aidha amewataka wananchi kutumia vizuri Vizimba vya kuhifadhia taka ili viweze kuleta maana iliyokusudiwa
“kama unavyoona hapa ambapo tunafanya usafi Kizimba kipo lakini bado mtu anakuja anaweka taka zake nje matokeo yake kama unavyoona zina ziba njia na inakuwa mazoea mtu afiki pale kwenye kizimba wanazitupa tu hapa nje” alisema Kagina.
Pia amewashukuru Wananchi na watumishi kwa kujitokeza kufanya usafi licha ya kuwa ni siku ya mapumziko na kuwaomba waendelee na mioyo hiyo ya kizalendo.
“Nashukuru muitikio umekuwa mzuri watumishi na wananchi wamejitokeza kwa wingi wakiongozwa na Mkurugenzi wetu, licha ya kuwa siku ya mapumziko lakini wamejitokeza kwa wingi wao na naomba tuendelee na morali hii pia kwa changamoto zilizojitokeza tutazifanyia kazi na siku za usoni hazitojirudia tena” alihitimisha Kagina
Zoezi la ufanyaji usafi katika viunga mbali mbali vya Mji wa kilwa masoko lilijumuisha wananchi na taasisi mbalimbali za kiserikali ikiwemo Benki ya Nmb tawi la Kilwa.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa