Uongozi wa Kitongoji Cha Masoko na Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wamefanya Mkutano na Wananchi wa Kitongoji cha Masoko ili Kutambulisha na kupokea maoni juu Ujenzi wa Mradi wa Kizimba cha Taka na Ukarabati wa Soko la Kilwa Masoko ili kuweza kustawisha huduma za Kijamii katika Soko hilo.
Mkutano huo umefanyika Tarehe 21/03/2025 katika Maeneo ya Soko la Kilwa Masoko ambapo Kaimu Mtendaji Kata ya Masoko Ndg.Tumpe Ndidi amesema Serikali imetoa Bajeti ya fedha Shilingi Milioni 25 kwaajiri ya Ujenzi wa Kizimba Cha Taka katika Soko hilo na Shilingi Milioni 50 ambapo mpaka saa Shilingi Milioni 20 za kwanza zimeingizwa kwenye akaunti ya Kata kwaajiri ya Ukarabati wa Soko hilo.
Akifafanua Hatua za Mwanzo za Ujenzi wa Kizimba Hicho Afisa Mazingira wa Wilaya Ndg. Boniface Achiula amesema Kizimba kitakachojengwa kitasaidia katika Uhifadhi wa Takataka na kufanya Mazingira ya Soko hilo kuwa Safi na Salama kwa Afya za Watumiaji, Pia amesema kitasaidia katika uhifadhi na usimamizi rahisi wa taka kutokana na kuwepo na vihifadhio Vidogo vidogo kisha kupeleka kwenye Kizimba kwaajiri ya kuhifadhiwa na baada ya muda kutupwa kwenye dampo Maalum, lengo ikiwa ni kuimarisha usafi wa Mazingira.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa