Katika jitihada za kukuza Kilimo na Maendeleo ya Jamii kwa Ujumla, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa yakabidhi Takribani Miche 15,000 ya minazi mbegu aina ya East African tall kwa wakulima wa minazi Wilayani Kilwa kupitia Wizara ya Kilimo, Jambi hili ni moja ya mpango wa serikali ya awamu ya sita wa kuwainua wakulima wa minazi Mkoani Lindi, ambapo Jumla ya miche 60,000 imetolewa Mkoani Lindi.
Akiwa katika zoezi la usambazaji wa miche hiyo, leo tarehe 27 Januari 2025 Afisa Kilimo Wilayani Kilwa Ndg.Kassim Kambwily, Amesema mbegu hizo zina ubora mkubwa wa kuvumilia magonjwa kwa muda mrefu, zinao uwezo mkubwa wa kuzaa na zina uwezo mkubwa wa kuishi kwa muda mrefu ukilinganisha na mbegu za miche nyingine.
Aidha Ndg. Kambwily amesema Serikali imetoa mbegu hizo bure kwa wananchi lengo ikiwa ni kuzalisha na kujipatia kipato hivyo amewataka wakulima wa Minazi hiyo, kufanya maandalizi na utunzaji mzuri wa mimea hiyo ili wapate kufaidika zaidi na kufikia malengo sahihi yaliyoadhimiwa na Serikali.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa