MHE. TELACK: " KAMILISHENI UJENZI WA MIRADI YA ELIMU KABLA YA TAREHE 29 JULAI 2023."
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa maelekezo hayo jumatatu ya tarehe 19 Juni 2023 katika kikao chake na Maafisa elimu wa Wilaya na Mkoa kwa ngazi za msingi na sekondari kilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi yake.
Akizungumza na Maafisa hao, Mhe. Telack amewataka Maafisa hao kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya miundombinu ya elimu hasa inayojengwa kupitia mradi wa BOOST.
Mhe. Telack amesema kuwa miradi yote ya ujenzi inayotekelezwa chini ya mradi wa BOOST iwe imekamilika na kukabidhiwa kwake kabla ya kufikia tarehe 29 Julai 2023. Ameongeza kuwa kukamilika kwa wakati kutawaepusha wanafunzi kupata matatizo ya afya itakayosababishwa na harufu za rangi za majengo.
Mhe. Telack amesema hakuna sababu ya kutokamilika kwa miradi hiyo kwa wakati Kwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekwisha toa fedha Kwa ajili ya utekelezaji.
Aidha, amewataka Maafisa elimu kuzingatia maelekezo yanayotolewa na viongozi wa mkoa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wakati.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa