Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (CMT), Tarehe 23/03/2025 imeendelea na ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Kata 23 za Wilaya hiyo, Ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha miradi yote inatekelezwa kwa ufanisi na viwango vinavyostahili. Ili kuhakikisha kata zote zinatembelewa kwa wakati, Timu hiyo imejigawa katika makundi matatu, ambapo kila kundi limepewa jukumu la kukagua miradi katika Kata zilizopangwa.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni umaliziaji wa nyumba ya walimu wenye thamani ya Tsh. 48,000,000/=pamoja na ujezi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Mbate wenye thamani ya Tsh. 18,000,000/= zote ni fedha kutoka mapato ya ndani, Pia ujenzi wa Ujenzi wa shule mpya ya Msingi eneo la Mihina (ujenzi wa vyumba 4 na matundu 2 ya vyoo) wenye thamani ya Tsh.100,000,000/= ikiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani, Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi Matandu wenye thamani ya Tshs. 48,000,000/= fedha kutoka mapato ya ndani.
Aidha, Timu imefanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa matundu 10 ya vyoo katika Shule ya msingi Namayuni wenye thamani ya Tsh.11,000,000/= fedha kutoka mapato ya ndani, Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya msingi Naipuli wenye thamani ya Tsh. 40,000,000/= fedha kutoka mapato ya ndani, na ujenzi wa nyumba ya mwalimu Shule ya msingi Masaninga wenye thamani ya Tsh.28,881,860.01/= fedha kutoka Mfuko wa Elimu.
Katika ziara hiyo, viongozi wa Timu ya menejimenti wamepongeza juhudi zinazofanyika katika utekelezaji wa miradi hiyo na kusisitiza umuhimu wa usimamizi mzuri wa rasilimali ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa. Ziara hiyo ni mwendelezo wa Mkakati wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa wa kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa haraka na kwa tija, sambamba na malengo ya serikali ya kuimarisha huduma za kijamii na miundombinu bora katika ngazi za jamii.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa