Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa na Utawala Bora imekabidhi Cheti Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa kutambua na kuthamani mchango wa Mkoa wa Lindi katika utoaji wa elimu na huduma kwenye maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma 2025.
Cheti hicho kimekabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwaniaba ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi wa maadhimiaho hayo.
Aidha, katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amewapongeza wawakilishi wa watumishi ambao wameshiriki maadhimisho hayo yaliyoanza Juni 16 hadi 23, 2025 katika viwanja vya Chinangali Dodoma huku akiwasisitiza kwenda kuyafanyia kazi na kuwafahamisha wengine yale yote ambayo wamejifunza kutoka katika viwanja hivyo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa