Kilwa,
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amesema hawezi kuvumilia kuona watu wana cheza pool table na michezo mingine muda wa kazi na kurudisha nyuma jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli za kutaka watu wafanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Ameyasema hayo alipokua akihutubia wakazi wa kijiji cha Mavuji baada ya kusimama kjijini hapo akiwa katika msafara kufuatia kitendao cha baadhi ya vijana kukutwa wakicheza mchezo wa pool table.
Amesema atawakamata wote ambao watakiuka agizo la kutocheza pooltable na michezo mingine muda wa kazi na kuwapeleka katika vyombo cha sheria.
“Ndugu zangu Sasa hivi ni saa 4 asubuhi na hawa vijana wanacheza pooltable kazi wanafanya saa ngapi?
Hatuwezi kwenda namna hii muda ambao wameruhusiwa kucheza michezo hii unajulikana sasa inakuwaje muda huu ambao wanatakiwa kufanya kazi wao wana cheza pool table” alihoji Zambi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mavuji baada ya kupita kijijini hapo na kukuta Vijana wakicheza Poool Table asubuhi kinyume na utaratibu uliowekwa (Picha :Ally Raumbo)
Aidha ameagiza kufungwa kwa vibanda ambavyo vinaendesha michezo ya bahati nasibu Maarufu kama Mabonanza na kuvisajiri kisheria.
“Wananchi hivi sio vitu vya kufumbia macho kabisa kwa sababu wanaoharibikiwa ni watoto wetu sasa naagiza kufungwa kwa vibanda ambavyo vinaendesha michezo ya bahati nasibu anayetaka kuendelea na biashara hii akajisajiri atambulike kisheria
siku nyingine ambayo haina jina tukikuta wanaendelea na michezo hii muda wa kazi tutakamata wachezaji na washangiliaji wote” alihitimisha Zambi
Katika tukio hilo kijana mmoja alikamatwa na jeshi la polisi alipokua akicheza pool table muda ambao sio rasmi kwa mchezo huo.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa