Marafiki wa Elimu Wilayani Kilwa wamefanya kikao na wadau wa Elimu Wilayani humo lengo ikiwa ni kuwasilisha taarifa ya ufuatiliaji wa uwajibikaji wa jamii katika malezi ya makuzi ya Awali ya Watoto, uliofanya na Kikosi kazi cha Marafiki wa Elimu kilifutilia uelewa na uwajibikaji wa jamii katika malezi ,makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto katika Wilaya ya Kilwa katika kata Nne ambazo ni Kivinje,Masoko, Miteja na Tingi. Hatua hii itasaidia kujenga hamasa na uelewa wa makuzi na malezi bora kwa mtoto.
Kikao Hicho kimefanyika Tarehe 28/03/2025 katika Ukumbi wa Sultani Kilwa Masoko ambapo kikosi kazi cha ufuatiliaji kimesema utafiti huo umefanyika katika Ngazi ya Shule za Awali mfano kwa Wamiliki wa Vituo vya kulelea Watoto mchana, Zahanati, Vituo vya Afya na Wazazi, hii imesaidia kupata uelewa namna jamii inashiriki katika utekelezaji wa Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM)
Akiwasilisha taarifa hiyo mratibu wa kikosi hicho Ndg. George Kamota amesema kuna changamoto ya uelewa katika jamii juu ya malezi na makuzi ya awali ya Mtoto katika Nyanja mbalimbali ikiwemo lishe bora kwa Watoto wenye umri wa miaka (0-8), ulinzi na Usalama wa mtoto mfano katika Usafiri wa watoto wadogo waendapo Shuleni kwa kutumia usafiri Kamavile usafiri Pikipiki
Mapendekezo yao juu ya Changamoto hizo ni wananchi wapewe Elimu juu ya Umuhimu wa Lishe kwa Watoto ili waweze kujifunza na kupunguza udumavu, Ulinzi na Usalama wa watoto upewe kipaumbele juu ya kuwafundisha Watoto kujilinda na ukatili, pia Vyombo vya usafiri waendesha pikipiki wazingatie usalama wa watoto wadogo.
Hata hivyo Ndg. Swahaba Matajiri akimuwakilisha Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa amewahasa wadau wa Elimu waliohudhuria kikao hicho kuieleimisha jamii juu ya kushirikiana katika malezi ya Mtoto kwa pamoja bila kubaguana. Kama kauli isemayo “ Mtoto wa mwenzio muone kama Mtoto wako
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa