Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) Wilaya wamejipanga kuhakikisha wanatatua changamoto ya upatikanaji wa maji Wilayani Kilwa ikiwemo uchimbaji wa visima virefu, uwekaji wa matenki katika vijiji vyenye changamoto ya maji
Hayo yamezungumzwa na Meneja wa RUWASA Wilayani humo Eng.Ramadhan Mabula alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya Maji katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kilichofanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri wa wilaya hiyo, ambapo amesema kuwa kwa sasa takribani ya Vijiji 62 kati ya vijiji 94 vilivyopo wilayani humo vinapata huduma ya maji safi na salama
Aidha Mabula amesema kuwa Wilaya inauhitaji wa Lita za maji 12,187,380 hata hivyo hadi sasa wamefanikiwa kusambaza Lita 7,617,112.5 na uwekaji wa mtandao wa Mabomba ya maji yenye 133Km ambapo kuna upungufu wa Lita 4,570,267.5 kwa Wilaya nzima, Hivyo takwimu hizo zinafanya 63.7% ya Wananchi wanapata maji safi na salama kwa sehemu za mjini na vijijini.
Hata hivyo, Meneja huyo amesema kuwa Bajeti ya mwaka 2023\2024 ambayo ni 2.7B itasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika vijiji mbalimbali vya Wilaya hiyo ikiwemo Nakiu,Kisimamkika,Zingakibaoni,Kinjumbi,Pandeplot n.k
Vilevile,amewasistiza watumiaji wa maji ambao ni wateja kulipa bili za maji kwa wakati ili kufanikisha zaidi huduma ya upatikanaji wa maji kwa maeneo mengine ambayo hayana maji kabisa
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ndg. Hanan Bafagih amempongeza Meneja wa RUWASA kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha Wananchi wote wilayani humo wanapata huduma ya maji safi na salama
Aidha,amemshukuru Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi anazotenga kwa ajili ya kutatua changamoto yam aji kwa wananchi hususani katika suala la kumtua ndoo Mama kichwani.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa