Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George B. Simbachawene amesema Maliasili na fursa zilizopo katika Mkoa wa Lindi, ziakisi maisha halisi ya wananchi Mkoani Lindi.
Mhe. Simbachawene ameyasema hayo alipotembelea Banda la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Jijini Dodoma tarehe 17 Juni, 2025.
Aidha Mhe. Simbachawene amesema Mkoa wa Lindi unayo mapato mengi yanayotokana na Korosho, ufuta, bahari na madini, hivyo Maliasili hizo zitumike vyema ili kuboresha maisha ya wananchi Mkoani Lindi.
Maadhimisho haya yaliyoanza tarehe 16 Juni 2025, yatahitimishwa tarehe 23 Juni 2025.
Kaulimbiu ya maadhimisho haya ni,
"Himiza matumizi ya mifumo ya kidigitali, kuongeza upatikanaji wa taarifa na Kuchagiza uwajibikaji"
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa