Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo chama cha Mapinduzi (CCM) CPA. Amosi Makala ametoa Pongezi kwa Waziri wa Ujenzi Ulega, TANROAD Mkoani Lindi na Uongozi wa Mkoa wa huo kwa kuhakikisha wanarudisha mawasiliano ya barabara kwa haraka tangu yalipotokea Maafa katika daraja la Somanga na Matandu ambapo madaraja hayo yaliathirika kwa Mvua katika siku za hivi karibuni.
Ametembelea eneo hilo na kujionea Jitihada hizo leo Tarehe 10/4/2025 alipokuwa katika Ziara yake Mkoa wa Lindi ambapo ameanzia katika Wilaya ya Kilwa, pia amepata nafasi ya Kuwasalimia wakazi wa kata ya Somanga na kuwapa pole kwa kadhia hiyo iloyojitoleza siku za hivi karibuni na kuwataka kuendelea kuwa na Imani na serikali hiyo ya awamu ya Sita juu ya jitihada wanazozifanya katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande waziri wa Ujenzi Mhe. Ulega amesema jitihada hizo za kurudisha mawasiliano katika eneo hilo yametokana na ushirikiano na umoja kutoka watalaamu,viongozi mkoani humo kwa kutumia muda Takribani siku Nne katika eneo hilo,hadi kuhakikisha magari yanaanza kupita katika eneo hilo kwa haraka tangu yalipotokea maafa hayo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telacky amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi cha Fedha Bilioni 100 kwaajiri ya ujenzi wa Madaraja yote yaliyoathirika katokana na mvua za mwaka jana na mpaka sasa wakamdarasi wote wapo katika maeneo hayo ya Ujenzi ili kuhakikisha wanatekeleza Ujenzi wa Miradi hiyo kwa viwango bora na muda uliokusudiwa
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa