Naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mhe. Jumaa Aweso ameuagiza uongozi wa Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini kufika na kufanya utafiti wa chanzo cha Maji kwa ajili ya kuchimba Kisima kitakacho saidia kuongeza upatikanaji wa Maji mjini Kilwa.
Agizo hilo amelitoa leo Disemba 8 wilayani Kilwa alipokuwa akihitimisha ziara ya siku moja wilayani humo baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya maji.
Aweso amesema wizara ya Maji imejipanga kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo ilani ya Chama cha mapinduzi ya kuhakikisha maji yanapatikana kwa asilimia themanini na tano vijijini na tisini na tano mjini ifikapo mwaka 2020 na kuwataka wakandarasi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ubora wa hali ya juu na kukamilisha miradi kwa wakati.
Amesema katika kuhakikisha tatizo la maji linakoma Mjini Kilwa wizara ya maji inatekeleza miradi katika Miji ishirini na sita ikiwemo Kilwa kupitia fedha za mkopo nafuu kutoka nchini india.
Aidha amewataka wakurugenzi watendaji kuwalipa wakandarasi kwa wakati pindi wapokeapo pesa kutoka wizarani.
Aweso amesema kuna baadhi ya wakurugenzi wamekuwa wakichelewesha malipo kwa wakandarasi baada ya kukamilisha miradi.
“Hata maandiko yanasema asiyefanya kazi na asile lakini kama mtu akifanya kazi ni haki yake kula, sasa kama mkandarasi amemeliza kazi yake kwanini asilipwe pesa yake kwa kazi ailiyofanya” alisisitiza Aweso
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilwa Mhe. Christopher Ngubiagai amewatahadharisha wananchi wanao ihujumu miradi ya maji kwa kufanya uharibifu kwa kukata mabomba na kuiba koki katika sehemu za kukingia maji kuacha mara moja.
Nguniagai amesema watafanya oparesheni maalumu katika vijiji vyote ambavyo vimekuwa vikiharibu miundo mbinu kwa makusudi na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote.
Awali akitoa taarifa kwa Naibu waziri wa Maji na umwagiliaji Meneja wa Mamlaka ya maji Kilwa masoko Mhandisi Issa Banda amesema kwa sasa Mamlaka ya maji mji wa kilwa inazlisha maji Mitakyubiki 934 mpaka mitakyubiki 1500 kwa siku na mahitaji halisi ni 2270 mpaka 2600.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa