Kilwa,
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa limepitisha Mpango wa matumizi ya Ardhi kwa vijiji vya Kikole, Kisangi,Mitole, na Kipindimbi pamoja na Sheria ndogo za kusimamia Mpango huo.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya uchambuzi na maelezo ya kina kutoka kwa Timu ya matumizi ya Ardhi wilaya ya kilwa kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya mipango na matumizi ya ardhi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichokaa Juni 13 kujadili mpango huo katika ukumbi wa Jumba la maendeleo Mjini Kilwa Masoko.
Baraza limesema limeridhia na kupitisha mpango na kuruhusu uendelee kwa hatua inayofuata
Mmoja wa wawezeshaji kutoka Timu ya matumizi ya Ardhi akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Madiwani na wakuu wa Idara wakati wa uwasilishaji wa mpango wa matumizi ya Ardhi kwa vijiji vya Kisangi, Mitole,Kipindimbi na Kikole katika baraza la madiwani lililo fanyika katika ukumbi wa jumba la maenedeleo kilwa masoko (Picha: Ally Ruambo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya kilwa Bw. Zablon Bugingo na Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira Halmashauri ya wilaya ya Kilwa Mhe. Msati wameishukuru na kuipoongeza timu iliyofanikisha kukamilika kwa mpango huo licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali.
“Ukisikiliza maelezo yao jinsi walivyopambana kufanikisha mpango huu hakuna neno la ziada unaloweza kuwapa zaidi ya Hongera, kwa mujibu ya maelezo yao moja ya changamoto ambayo waliyokutana nayo ni kunaswa kwa mmoja wao katika mtego ambao ulitegwa kwa ajili ya kumnasa Nyati sasa unaweza kuona ugumu wa kazi ulivyokuwa” alisema Bugingo.
Madiwani na wakuu wa Idara wakifuatilia kwa umakini wa uwasilishwaji wa mpango wa matumizi ya Ardhi kwa vijiji vya Kisangi, Mitole,Kipindimbi na Kikole katika kikao kilichofanyika fanyika katika ukumbi wa jumba la maenedeleo kilwa masoko (Picha: Ally Ruambo).
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa