LINDI YANDELEZA UBABE MASHINDANO UMITASHUMTA 2019
Na David Langa-Mtwara
Timu za mkoa wa Lindi zinazoshiriki mashindano ya shule za msing kitaifa mwaka 2019 mkoani Mtwara zimeendeleza ushindi mkubwa dhidi ya timu pinzani.
Ikiwa ni siku ya tatu ya mashindano hayo , leo Timu za Mkoa wa Lindi zimeshinda kwa Kishindo katika michezo sita huku wakipata suluhu katika mchezo mmoja wa mpira wa miguu wavulana dhidi ya timu kutoka makoa wa Simiyu.
Michezo iliyochezwa leo ni mpira wa pete (Netball) dhidi ya Dodoma ambapo timu ya ya Mkoa wa Lindi iliichapa timu ya Dodoma magoli 20 kwa 11, mchezo mwingine ni mikono (Handball) dhidi ya Tabora ambapo Tabora ilichapwa goli tisa(9) kwa tano(5).
Michezo mingine ya siku ya leo ni mpira wa mikono (Handball) dhidi ya mkoa wa Kagera iliyomalizika kwa timu ya Mkoa wa Lindi kuichabanga timu ya Kagera jumla ya goli 13 kwa moja, huku katika mchezo wao mpira wa miguu kwa wasichana dhidi ya timu ya Ruvuma ikimalizika kwa ushindi wa jumla ya goli tano kwa sifuri.
Michezo hiyo inayoendea katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara inajumuhisha timu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.
Ushindi wa timu za Mkoa wa Lindi umechagizwa na maandalizi mazuri pamoja na hamasa kubwa wanayoipata wachezaji kutoka kwa viongozi wao kuanzia wakurugenzi, maafisa Elimu wa Wilaya zote pamoja na uongozi ngazi ya Mkoa ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Lindi Mhe.Godfrey Zambi.
Mwalimu wa mpira wa miguu wa Mkoa wa Lindi Mwl.Hamisi amethibitisha uwezo mkubwa wa timu yake na kuahidi ushindi mkubwa kwa mechi zijazo.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Bi.Rehema Madenge na Msaidizi wake Dr.Bora Haule wameendelea kutoa hamasa kwa walezi wa timu zote ikiwa ni pamoja na motisha kwa wachezaji katika kila mechi wanayoshinda jambo ambalo limengeza hari ya ushindi kwa timu zote.
Kilwa Masoko
Anuani ya Posta: 160
Simu: 0672365354
Simu: 0672581557
Barua pepe: ded@kilwadc.go.tz /ictsupport@kilwadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa